1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK : Urusi yatakiwa isitumie kura ya turufu

14 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBir

Marekani imeitaka Urusi kutopiga kura ya turufu dhidi ya azimio la Umoja wa Mataifa juu ya Kosovo kwa kusema kwamba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litaachwa bila ya kuwa na dhima katika mustakbali wa jimbo hilo.

Balozi wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa Zalmay Kalilzad amesema Marekani na nchi wanachama wa baraza hilo wa Umoja wa Ulaya wanataka kuona hatua zinachukuliwa kwa vitendo katika siku chache zijazo.Viongozi wa Kosovo wa asili ya Kialbania wamedokeza kwamba wanafikiria kujitangazia uhuru kutoka Serbia.

Anayetumika kama waziri wa mambo ya nje wa jimbo hilo Veton Surroi amesema Umoja wa Mataifa hauna njia tena ya kulipatia jimbo hilo uhuru kutokana na pingamizi ya Urusi kwa niaba ya mshirika wake Serbia.