1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK: Vikwazo vipya dhidi ya Iran

25 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCFZ

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limeidhinisha vikwazo vipya dhidi ya Iran inayokataa kusitisha mradi wake wa kurutubisha madini ya uranium.Balozi wa Uingereza,Sir Emyr Jones Parry alipozungumza kwa niaba ya nchi sita zilizopendekeza azimio hilo,alisisitiza azma yao ya kutaka kufanya majadiliano pamoja na Iran. Vikwazo hivi vipya vinazuia kufanya biashara ya silaha na Iran;hulenga benki ya taifa ya Iran-Bank Sepah na vile vile wakuu wa Walinzi wa Mapinduzi.Vikwazo hivi vinafuata azimio lililopitishwa Desemba mwaka jana,kupiga marufuku biashara inayohusika na zana za kinyuklia pamoja na makombora.Vile vile pesa za watu binafsi na za taasisi zilizohusika na miradi ya nyuklia zimezuiliwa.