1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Azimio la vikwazo dhidi ya Iran linajadiliwa na baraza la usalama

21 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CChb

Baraza la usalama la Umoja wa mataifa linajadili azimio linalotaka Iran iwekewe vikwazo kuhusiana na mpango wake wa Kinuklia unaotuhumiwa na umoja wa Ulaya kuwa wa kutengeneza silaha hatari.

Uingereza,Ufaransa na Ujerumani zimejaribu kuutuliza wasiwasi wa Urussi na China kuhusu vikwazo vya usafiri dhidi ya wanasiasa,viongozi wa kibiashara na watu 12 wanaohusika katika mpango huo wa Kinuklia wa Iran.

Marekani pamoja na nchi hizo tatu za Umoja wa Ulaya wanatarajia mswaada huo utapigiwa kura hapo kesho.Endapo azimio hilo litaidhinishwa Iran itapigwa marufuku kuingiza au kusafirisha bidhaa na technologia inayohusiana na urutubishaji wa madini ya Uranium na elimu kuhusu utumiaji wa makombora.

Iran imetishia kulipiza kisasi endapo azimio hilo litapitishwa.