1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW-YORK:Ban Ki-Moon amtuma mjumbe maalum jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo

1 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ap

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon ametuma mjumbe maalum katika jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ajili ya mazungumzo ya kuutatua mgogoro nchini humo kufuatia kuongezeka kwa mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali.

Msaidizi wa katibu mkuu anayehusika na masuala ya kisiasa Haile Menkerious ameondoka hapo jana kuelekea nchini humo kukutana na viongozi wa serikali halkadhalika viongozi wa nchi za eneo hilo.

Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo MONUC pamoja na jeshi la serikali wamefahamisha kwamba kumekuwepo na mapigano mapya katika jimbo la Kivu kaskazini kati ya wanajeshi na waasi wanaongozwa na Generali muasi Laurent Nkunda.Mapigano hayo ndio ya kwanza kwenye eneo hilo katika muda wa siku 10 na tangu rais Joseph Kabila alipotoa ruhusa kwa wanajeshi wake kutumia nguvu kuwanyan’ganya silaha waasi hao endapo wanakataa kusalimu amri ifikiapo mwishoni mwa mwaka.