1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Katibu mkuu alaani mauaji ya askari huko Darfur

1 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/CBL9

Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki Moon amelaani mauaji ya askari 10 wa jeshi la umoja wa Afrika linalolinda amani katika jimbo la Darfur nchini Sudan.

Askari hao walivamiwa mwishoni mwa wiki na watu ambao hadi sasa hawaja tambulika.

Katika shambulio hilo lililo tokea kwenye kituo cha Haskanita, wanajeshi wanane walijeruhiwa na wengine arobaini hawajulikani walipo.

Wanajeshi hao wameuwawa wakati ambapo mazungumzo ya kutafuta amani yanatarajiwa kufanyika nchini Libya mwishoni mwa mwezi huu.

Lengo la mazungumzo hayo ni kuzishirikisha pande zote zinazo husika na mgogoro wa jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan.

Wakati huo huo ujumbe wa kimataifa unao ongozwa na askofu mkuu Desmond Tutu wa Afrika Kusini unatarajiwa kufanya mazungumzo na rais Omar El Bashir wa Sudan.

Ujumbe huo pia utakutana na wawakilishi wa upinzani kabla ya kuelekea kwenye kambi za wakimbizi katika jimbo la Darfur.