1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Ndege yaangukia katika nyumba ya mastakimu,wawili wafa

12 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3d

Ngede ndogo ya mtu binafsi imeangukia katika jengo moja refu la mastakimu mjini New York na watu wawili wamekufa.

Ndege hiyo ilikuwa mali ya mcheza Baseball wa timu ya New York Yankees Cory Lidle aliekuwa rubani wakati ajali hiyo ilipotokea. Lidle pamoja na mtu mwingine walikufa katika ajali hiyo.

Idara za usalama za mjini New York zimesema , hakuna dalili za matendo ya kigaidi .