1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Rais wa Iran akatazwa kuingia Ground Zero

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOJ

Uongozi mjini Newyork unakataa kuidhinisha ombi la Rais wa Iran Mahmoud Ahmedinejad la kuzuru eneo la Ground Zero wiki ijayo lililoko Manhattan kulikotokea mashambulio ya mwezi Septemba 11 mwaka 2001.Ombi hilo linakataliwa kwasababu za kiusalama aidha ukarabati unaoendelea palipokuwa na majengo ya World Trade Centre.

Kiongozi huyo alitaka kuzuru eneo hilo akiwa katika safari rasmi ya kuhudhuria kikao cha Baraza la Umoja wa mataifa kinachopangwa kufanyika juma lijalo.Ombi hilo lilikataliwa baada ya mkutano wa maafisa wa idara ya polisi ,ujasusi na Mamlaka ya Bandari ya Newyork na New Jersey inayosimamia eneo hilo.Mgombea wa urais wa chama cha Republic layekuwa meya wa mji huo wakati wa shambulio hilo Rudolph Giuliani alishawishi uongozi wa mji kukataa kutimiza ombi hilo.

Rais Ahmedinejad anatarajiwa kuhutubia Baraza la Umoja wa Mataifa siku moja pamoja na Rais Bush wa Marekani jumanne ijayo.Ziara ya Rais Ahmedinejad inapangwa kufanyika wakati uhusiano kati ya Iran na Marekani si mzuri kwasababu ya mpango wa nuklia wa Iran unaozua utata.