1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:Umoja wa mataifa waanzisha juhudi mpya za amani Darfour

6 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcr

New-York:

Umoja wa mataifa na umoja wa Afrika wametangaza utaratibu mpya wa amani kwa mzozo wa jimbo la Darfour nchini Sudan.Mjumbe maalum wa umoja wa mataifa katika jimbo la Darfour,Jan Eliasson anapanga kulitembelea eneo hilo mwishoni mwa mwezi huu, kujaribu kuzuwia mapigano kati ya makundi ya waasi na vikosi vya serikali ya Sudan.Bwana Jan Eliasson amesema lengo la utaratibu huu mpya ni kufufua mazungumzo kati ya pande zinazohusika.Kabla ya hapo mjumbe huyo maalum wa Umoja wa mataifa na muakilishi wa Umoja wa afrika,Salim Ahmed Salim walikutana na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-Mooon mjini New-York.Kwa upande wake Marekani inajitahidi kuishawishi jamhuri ya umma wa China ikubali kushiriki katika juhudi za upatanishi za Darfour.Makubaliano ya amani yalitiwa saini mwezi May uliopita kati ya serikali na kundi moja kuu la waasi,lakini matumizi ya nguvu yamekua yakiendelea huku makundi mengine ya waasi yakipinga kutia saini makubaliano hayo.