1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NEW YORK:UN yamuidhinisha mnywarwanda kuongoza jeshi lake Darfur

18 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBOn

Umoja wa Mataifa umekubaliana na uteuzi wa afisa wa juu ya kijeshi wa Rwanda kuwa kaimu kamanda wa kikosi cha Umoja wa huo cha kulinda amani kwenye eneo lenye mzozo la Darfur.

Hiyo ni baada ya kutokuwepo kwa ushahidi wa kutosha juu ya shutma zilizotolewa dhidi ya afisa huyo Meja Jenerali Karenzi Karake ya kuhusika na uhalifu wa dhidi ya haki za binaadamu.

Jenerali Karake anachukua nafasi hiyo kujaribu kusimamia uundwaji wa jeshi la pamoja kati ya lile la Umoja wa Mataifa na la Umoja wa Afrika katika eneo hilo.Rwanda ina askari kiasi cha elfu mbili kati ya elfu 7 wa Umoja wa Afrika katika eneo hilo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Michele Montas amesema kuwa uteuzi wa Jenerali Karake utaendelea kama kawaida kwa sababu hakuna ushahidi wa kutosha juu ya shutma zilizoelekezwa kwake.

Jean –Baptise Mbera Bahizi ambaye ni Katibu Mkuu mkuu wa kundi la upinzani la United Demokratic Forces lililouhamishoni nchini Ubelgiji alidai kuwa General Karake alisimamia hukumu za mauaji ya watu kabla na baada ya majeshi ya RPF kutwaa madaraka nchini Rwanda kufuatia mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.