1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ni nani atakayekuwa bingwa wa Ulaya

27 Mei 2011

Manchester United na Barcelona, zinakutana katika fainali za 11 za mashindano ya Champions league, uwanjani Wembley.

https://p.dw.com/p/11PRs
Miamba ya soka ya Uingereza na Uhispania inapania kudhihirisha umahiri wao uwanjani WembleyPicha: picture alliance/empics

Mafahali wawili wanasubiriwa kwa hamu kuteremka dimbani katika mechi ya kufa au kupona na hatimae kuchukua taji la ubingwa barani Ulaya.

Symbolbild Champions League Finale 2011
Manchester United na Barcelona, ni nani aliye bingwa?Picha: DW/AP/UEFA

Safari ya Uingereza huwa kwa kawaida sio ya rahisi kwa Mashetani wekundu Manchester united ambao mara nyingi huishia kufungwa kwao, ambao hali yao ni sawa na timu pinzani Barcelona ilioshindwa na Arsenal mara ya mwisho iliposafiri kwenda Uingereza.

Lakini Man U inataraji kuwa kucheza kwao leo Wembley huenda kukawapa faida dhidi ya wapinzani wao.

Historia ya kombe hilo inaonesha kuwa timu zilizocheza nyumbani zililishinda mara saba kombe hilo.

Ushindi huo unajumuisha wa kwanza wa Machester United dhidi ya Benfica mnamo mwaka 1968 katika uwanja wa zamani wa Wembley, walikomaliza kwa ushindi wa mabao 4-1 katika muda wa ziada.

Timu nyenginezo zilizochukuwa ushindi nyumbani ni pamoja na Real Madrid mwaka 1957, AC Milan 1965, Ajax 1972, Liverpool 1978, Juventus 1996, na Borussia Dortmund 1997.

Lakini Stade de Reims 1956, AS Roma 1984, na Barcelona 1986 zote zilifungwa kwenye fainali hizo nyumbani.

Mwanasoka mashuhuri Ujerumani Franz Beckenbauer anaamini kuwa siku zote ni faida kwa timu ikiwa inashiriki mashindano ikiwa nyumbani.

Anasema imekuwa kama utamaduni kuwa timu nyingi za Uingereza zinakuwa na nguvu zinapocheza nyumbani kuliko katika eneo jingine Ulaya, na kwa upande mwingine Barcelona haijashughulika kamwe kuhusu wapi wana uwezo wa kufanya miujiza yake.

Norman Foster Wembley Stadion London
Uwanja wa Wembley uliopo kaskazini magharibi mwa LondonPicha: AP

Huenda Manchester vile vile ikapata morali kujuwa kuwa timu ya Liverpool pia ilishinda taji lake mnamo mwaka 1978 uwanjani Wembley, kwa kuifunga Club Brugge 1-0. Hatahivyo Barcelona pia ina kumbu kumbu nzuri ya fainali ya mwaka 1992 uwanjani umo humo, walipoifunga Sampdoria katika muda wa ziada.

Kocha wa Barca, Pep Guardiola amesema kuwa anaamini kucheza uwanjani Wembley kutaipa faida Manchester, kwa kuwa timu hiyo hucheza katika uwanja huo, na huwa timu inastarehe inapocheza nyumbani.

Lakini Guardiola anasema kuwa hili sio tatizo wala tishio kwa Barcelona maana walilitambua hili tangu mwanzo wa msimu wa mashindano haya.

Der Trainer von Barcelona Pep Guardiola
Kocha Pep Guardiola wa timu ya BarcelonaPicha: AP

Rekodi ya Barcelona katika michezo ya kukaribishwa na timu pinzani za Uingereza inadhihirisha kuwa sio nzuri, maana imefanikiwa kushinda mara 6, kutoka sare mara 8, na imeshindwa mara 13. Huku rekodi yao dhidi ya timu za Uingereza mjini London inaonesha kuwa Barca imeshinda mara 2, imetoka sare mara 3, na imeshindwa mara 4.

Hatahivyo timu hiyo ya Catalan, ina utaalamu wa kuwafunga wapinzani wake wa Uingereza uwanjani humo Wembley, kwa mfano ushindi wake dhidi ya Arsenal katika kiwango cha makundi msimu wa 1999/2000 ushindi wa mabao 4-2.

Hii ni mechi ya 11 dhidi ya timu hizi mbili zikiwa na ushindi mara tatu kila mmoja, na zimetoka sare katika mechi nne. Ushindi wa Barcelona wa mabao 2-0 dhidi ya Manchester united kwenye fainali za mwaka 2009, ndio lilikuwa pambano lao la mwisho.

Mwandishi: Maryam Abdalla/DPAE
Mhariri:Abdul-Rahman