1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nicosia. Tetemeko laikumba Cyprus.

15 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2W

Tetemeko la ardhi asubuhi ya leo lililo katika kiwango cha 4.7 katika kipimo cha Richter limelikumba eneo la pwani katika kisiwa cha Cyprus kilichoko katika bahari ya Mediterranean.

Tetemeko hilo , ambalo limetokea mapema leo asubuhi , limekuja wakati mmoja ambapo kulikuwa na radi na ngurumo.

Watu walioshuhudia wamesema kuwa tetemeko hilo limedumu kwa muda wa sekunde 20. Polisi wamesema kuwa hakuna ripoti za majeruhi ama majengo yaliyoporomoka.