1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria: Kundi la Niger Delta kushambulia sekta ya mafuta

17 Januari 2018

Kundi hilo limesema mashambulizi hayo yatakuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea

https://p.dw.com/p/2qyr8
Nigeria Militär-Patrouillen im Niger-Delta
Picha: DW/M. Bello

Kundi la Nigeria la wapiganaji wa Niger Delta Avengers limesema leo kuwa litaanzisha mashambulizi dhidi ya sekta ya mafuta nchini humo katika siku chache zijazo.

Katika taarifa yake iliyoiweka kwenye tovuti kundi hilo limesema mashambulizi hayo yatakuwa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea na yatalenga operesheni za mataifa kadhaa katika eneo la bahari kubwa.

Mnamo mwezi Novemba kundi hilo ambalo limeshambulia vituo kadhaa vya mafuta mwaka 2016 lilisema kuwa limesimamisha makubaliano ya kusitisha mapigano.