1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria kuumana na Tahiti

18 Juni 2013

Mgogoro kuhusu marupurupu ambao ulitishia ushiriki wa Nigeria katika kinyang'anyiro cha FIFA cha kombe la mabara – FIFA Confederations Cup, kinachoendelea nchini Brazil ni kama haujatuliwa kikamilifu.

https://p.dw.com/p/18rCq
Nigeria's national football team players celebrate after winning the 2013 African Cup of Nations final against Burkina Faso on February 10, 2013 at Soccer City stadium in Johannesburg. AFP PHOTO / BEN STANSALL (Photo credit should read BEN STANSALL/AFP/Getty Images)
Sport Fußball Africa Cup of Nations 2013 Finale Nigeria Burkina FasoPicha: Getty Images

Nahodha wa kikosi cha Super Eagles Vincent Enyeama amesema mzozo huo ambao ulionekana kusuluhishwa Ijumaa iliyopita, umetatuliwa tu kwa sasa. Vijana hao wa kocha Stephen Keshi wametua mapema jana nchini Brazil na hii leo wanafungua kampeni yao kwa kupambana na Tahiti. Enyeama amesema Mzozo huo wa mishahara na marupurupu ya wachezaji uliendelea hadi siku nne za mwisho kabla ya wao kusafiri, na kwa sasa hawataki kuuzungumzia.

Wachezaji wa Nigeria waliahidiwa dola 10,000 kwa kila mechi watakayoshinda katika kinayang'anyiro hicho, na dola 5,000 kwa kila mechi watakayotoka sare, lakini shirikisho la soka Nigeria NFA lilisema kabla ya kikosi hicho kulekea Brazil, kuwa haliwezi kumudu kiwango hicho cha marupurupu na sasa kitapunguza kwa nusu. Wachezaji wa Nigeria walikataa kuondoka hotelini mjini Windhoek, Namibia walikotoka sare na wenyeji katika mchuano wa kufuzu katika kombe la dunia.

Mabingwa wa Ulimwengu Uhispania walionyesha "tiki taka" na kuwatuliza mahasimu wao Uruguay
Mabingwa wa Ulimwengu Uhispania walionyesha "tiki taka" na kuwatuliza mahasimu wao UruguayPicha: Reuters

Katika mechi zilizochezwa jana, mabingwa wa ulimwengu Uhispania waliwazidi nguzu Uruguay mabao mawili kwa moja, wakati Italia pia ikiwazaba Mexico magoli mawili kwa moja. Kombora la Pedro lililomgonga beki wa Uruguay Diego Lugano na Pedro Soladado yaliwapa mwanzo bora Uhispania wakati Luiz Suarez akaifungia Uruguay goli safi kwa njia ya freekick. Mario Balotelli na Andrea Pirlo waliifungia Italia magoli mawili wakati Javier “Chicharito” Hernandez akiwafungia Mexico goli moja.

Na wakati mechi za kombe la mashirikisho zikiendelea nchini Brazil, na pia nchi hiyo ikiendelea na maandalizi ya viwanja vitakavyotumiwa katika fainali za dimba la dunia hapo mwakani, mataifa mengine nayo yanaendelea kutafuta tikiti na kuhakikisha kuwa yanashirki katika dimba hilo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman