1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria: Uchaguzi unaogubikwa na rushwa na upambe.

Sekione Kitojo2 Aprili 2007

Ni wakati wa kumwaga fedha katika nyumba ya mwanasiasa wa Nigeria Lamidi Adedibu ,na eneo la kuegesha magari nyumbani kwake limejaa watu ambao wanashauku ya kupata angalau fedha kidogo. Huu ni wakati wa kukaribia uchaguzi nchini Nigeria na hali hii ni ya kawaida kabisa. Uchaguzi nchini Nigeria hugubikwa na masuala ya rushwa na upambe.

https://p.dw.com/p/CHH2

Wakati Lamidi Adedibu akijitokeza kutoka nyumbani kwake, watu wanajipanga , wanawake wanapiga magoti, wapigaji ngoma wanazidisha mirindimo ya ngoma na mwimbaji mtoa sifa anamsifu kupitia kipaaza sauti kwa sauti ya juu kabisa.

Adedibu ambaye ni mtu mzima kidogo, ambaye atakuwa na jukumu la juu kabisa katika hatima ya uchaguzi wa mwezi huu katika jimbo atokako la kusini magharibi la Oyo, yuko na wasaidizi wake, wapambe ambao wameshikilia mifuko ya plastiki iliyojaa fedha. Anakaa chini , msaidizi akimpepe, na kazi inaendelea ya kugawa noti kwa umati wa watu waliojaa hapo kwa muda wa saa mbili nzima.

Mgao wa fedha ni mkakati wa kawaida unaotumiwa na wanasiasa nchini Nigeria, hususan wakati wa kuelekea katika uchaguzi. Kwa Wanigeria ambao waliochoshwa na miongo kadha ya ujali rushwa na kuporomoka kwa huduma muhimu za kijamii, ni nafasi ya kujipatia kitu halisi kutoka kwa wanasiasa wao, hata kama ni mabadiliko madogo.

Adedibu anatoa kiasi cha Naira 600 kwa mtu mmoja ikiwa ni sawa na dola tano. Mimi ni mtu wa watu, anasema , huku akitabasamu, wakati wa mahoajiano na shirika la habari la Reuters muda mfupi tu baada ya tukio la kugawa fedha mara mbili kila wiki. Amesema utajiri wake unatokana na biashara inayofanywa na familia yake.

Katika jimbo la Oyo, jimbo ambalo lina wakaazi wengi zaidi anaudhibiti licha ya kuwa hashiki wadhifa wowote rasmi, Adedibu anafahamika kwa majina mengi, mtu mwenye nguvu, chifu, jenerali, ama , kwa jina maarufu zaidi, kiongozi mbabe, ama Godfather.

Nimewasaidia wengi wa viongozi wetu na nataraji kuwa nao watanisaidia pia, anasema Adedibu.

Niko hapa kwa mapenzi ya watu, amesema .

Vipi anafahamu kuwa wanamsujudia.

Nigeria ikiwa ni nchi yenye wakaazi wengi zaidi barani Afrika , na muuzaji mkubwa wa mafuta ghafi, ilirejea katika demokrasia mwaka 1999 baada ya miongo mitatu ya mlolongo wa utawala wa wanajeshi.

Uchaguzi hapo Aprili 21 unatarajiwa kuadhimisha awamu ya kwanza ya mpito kutoka rais wa kwanza aliyechaguliwa hadi mwingine. Katika kinyang’anyiro cha hapo Aprili 14, viti 36 vya magavana wenye nguvu katika majimbo vitagombaniwa ikiwa ni pamoja na kiti cha jimbo la Oyo.

Lakini wanaharakati wa vyama vya kijamii wanasema kuwa Nigeria ni nchi ya kidemokrasia tu kwa jina , kwasababu wizi wa kura uliokithiri pamoja ghasia katika chaguzi za mwaka 2003, zilitoa kundi la viongozi ambao hawana uhalali wa kutawala. Hofu ni kwamba uchaguzi unaokuja unaweza kuingia doa kama hilo pia.

Katika muda wa miezi mitano iliyopita , vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti zaidi ya matukio 70 ya ghasia zinazohusiana na uchaguzi na kusababisha zaidi ya watu 70 kupoteza maisha.

Pia wanasiasa wanawalipa na kuwapa silaha makundi ya wahuni ili kuweza kufanya watakavyo kwa wapiga kura ama upande wa upinzani. Makundi hasimu mara kwa mara yanapambana kandoni mwa mikutano wa hadhara ya kampeni.

Ni vipi mtu anaweza kutaraji kuwa mpigakura atafanya maamuzi huru wakati wababe wanawapa silaha vijana wasio na kazi pamoja na mapanga ili kuwakorofisha?, amesema Mashood Erubami, mwanaharakati anayepambana kuimarisha demokrasia mjini Ibadan katika jimbo la Oyo.