1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nigeria yamkamata msemaji wa Jonathan

Daniel Gakuba
25 Oktoba 2016

Ofisi ya Kupambana na Rushwa ya Nigeria (EFCC) inasema imemtia nguvuni na kumuweka kizuizini msemaji wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Goodluck Jonathan, ikimtuhumu kwa ufisadi wakati akihudumu serikalini.

https://p.dw.com/p/2Rg8Z
Reuben Abati Sprecher des nigerianischen Präsidenten
Picha: DW/U. Musa

Duru kutoka ndani ya ofisi hiyo zimesema afisa huyo, Reuben Abati, anahusishwa na matumizi mabaya ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya kupambana na kundi la kijihadi la Boko Haram.

Msemaji wa EFCC, Wilson Uwuajeren, amesema Abati anahojiwa akiendelea kusalia kizuizini.

Kabla ya kuteuliwa kuwa msemaji wa Rais Jonathan, Abati alikuwa mwandishi maarufu na mwenyekiti wa bodi ya wahariri wa gazeti la Guardian la Nigeria.

Anatuhumiwa kupokea fedha kutoka mshauri wa zamani wa masuala ya usalama Sambo Saduki, ambaye pia anakabiliwa na tuhuma za mikataba hewa ya ununuzi wa silaha za kupambana na Boko Haram.