1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nini kitatokea zaidi baada ya kukamatwa Nkunda?

Sekione Kitojo23 Januari 2009

Laurent Nkunda amekamatwa na jeshi la Rwanda baada ya jeshi hilo kushutumiwa kwa muda mrefu kuwa lilikuwa likimsaidia katika mzozo wa mashariki ya Congo.

https://p.dw.com/p/Gf2f
Kiongozi wa zamani wa kundi la waasi la CNDP Laurent Nkunda ambaye amekamatwa hivi karibuni na jeshi la Rwanda huko Bunagana.Picha: AP

Laurent Nkunda na kundi lake la waasi walikuwa wanaonekana kuwa wanashirikiana pamoja na Rwanda katika mzozo wa eneo la mashariki ya Congo. Kwa muda wa miezi kadha umoja wa mataifa umekuwa ukilishutumu jeshi la Rwanda, kumsaidia jenerali huyo , ambaye alikuwa akipigana na majeshi ya serikali mjini Goma. Hivi sasa lakini pamoja na mambo yote jeshi la Rwanda siku ya Jumanne limemkamata jenerali Nkunda.



Kwa muda wa miaka kadha Laurent Nkunda alikuwa akionekana kuwa mshirika wa Rwanda katika mzozo wa mashariki ya Congo. Vifaa na fedha vinavyotumiwa na waasi wanaoongozwa na jenerali huyo, inasema serikali ya Kongo , vinatoka kwa nchi hiyo ndogo jirani.

Lakini hapo Alhamis wiki hii Nkunda alitiwa mbaroni. Na wale wale ambao walikuwa wakishutumiwa kumpa misaada. Msemaji wa ujumbe wa kulinda amani cwa umoja wa mataifa nchini Congo , MONUC Jean Paul Dietrich amesema.

Kwa taarifa nilizonazo ni kwamba Nkunda alikamatwa jioni ya Alhamis katika eneo la Bunagana, ambalo ni mpaka kati ya mashariki ya Congo na Rwanda, ikiwa ni kolometa 956 kaskazini ya mji wa Goma. Hadi sasa nafahamu kuwa amekamatwa na wanajeshi wa Rwanda.


Watu walioshuhudia katika eneo hilo wanaeleza kuwa kulitokea mapambano katika eneo la Bunagana jioni hiyo. Kabla ya hapo jeshi la Congo na lile la Rwanda , siku moja kabla walikuwa wakipambana na waasi mashariki ya Congo, wakimtaka Nkunda kujisalimisha. Nkunda alikimbia, na muda mfupi alikamatwa ndani ya ardhi ya Rwanda.


Waziri wa ulinzi wa Congo alimtaka Nkunda kuweka silaha chini na kusitisha shughuli zote za kundi hilo la waasi. Kukamatwa kwa Nkunda ni mafanikio ya kwanza ya ujumbe wa jeshi la Rwanda na Kongo likiwa na wanajeshi jumla wapatao 3,500. Hadi sasa viongozi wa majeshi yote wamesema tu kwamba wanawasaka wanamgambo wa Kihutu ambao wanahusika na mauaji ya halaiki nchini Rwanda. Kwa hivi sasa amekamatwa jenerali huyu wa Kitutsi, ambaye kwa kusema kuwa anawalinda Watutsi wachache kutokana na wauaji hao wa Kihutu amezidisha wasi wasi na mauaji katika eneo la mashariki ya Congo. Msemaji wa umoja wa mataifa Jean Paul Dietrich amesema.

Tunaweza kusema kwa kweli Nkunda hakuwa mtu wa amani, alikuwa na mambo yake. Tutaona iwapo juhudi zote zilizofanywa katika siku chache zilizopita, hususan na jeshi la CNDP kuweka chini silaha, zitaleta amani ya kudumu katika eneo hili.


Wapi anakoshikiliwa Nkunda hadi sasa bado hajajulikana hadi leo. Anapaswa hata hivyo kuwajibika na yale aliyoyafanya. Kutokana na kuendewa kinyume kwa kiasi kikubwa haki za binadamu anapaswa kupelekwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita mjini The Hague.

►◄