1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nkurunziza hatohudhuria mkutano wa Afrika Mashariki

18 Mei 2017

Rais wa Burundi hatohudhuria mkutano wa kilele wa marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki-EAC utakao fanyika jumamossi mjini Dar es salam. Nkurunziza atawakilishwa na makamu wake ambaye tayari ameondoka Bujumbura

https://p.dw.com/p/2dBwE
Burundi Pierre Nkurunziza und Denise Bucumi
Picha: picture-alliance/dpa/M. Reynolds

Hayo ni wakati watu 4 wameuwawa Bujumbura katika matokeo mawili tafauti. Kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura, kuelekea Dar Salam, makamu wa kwanza wa rais amewambia waandishi wa habari kuwa atamuakilisha rais Pierre Nkurunziza katika mkutano wa kilele wa 18 wa viongozi wa jumuia ya Afrika mashariki EAC.

Gaston sindimwo amesema mkutano huo si wakujadili swala la Burundi bali ni wa kila mwaka kwa ajili ya makadirio ya hatua zilopigwa katika utaratibu unaozihusisha  sekta mbali mbali katika nchi wanachama kama Soko huru na shirikisho la kisiasa.

East African Community Gipfel Tansania Arusha
Tangu jaribio la mapinduzi Burundi, Nkurunziza hasafiri njePicha: picture-alliance/dpa/Xinhua

Gaston Simwo anakwenda kumuwakilisha rais Nkurunziza wakati ndiye alotarajiwa kuhutubia katika mkutano huo wa marais. Makamu wa kwanza wa rais amesema pindi rais anapokuwa na majukumu mengi yanayo mkabili na kawaida kuwakilishwa. "Sielewi kwanini mnasema rais hakuitikia mkutano mimi kama na kwenda ni namuwakilisha yeye, rais na hata marais wengine pindi wanakuwa na makjukumu wengi huwatewa wengine wajumbe wa serikali kuwawawkilisha, kwa hiyo ni jambo la kawaida siyo tataizo".

Tangu kutokea jaribio la mapinduzi ya kijeshi yalofeli mei 13 2015 rais Nkurunziza akiwa katika mkutano wa kujadili mzozo wa Burundi, rais Nkurunziza hajawahi tena  kusafiri nje ya mipaka ya Burundi.

Hayo ni wakati watu wa 4 wameuwawa katika matokeo mawili tafauti. Kulingana na msemaji wa polisi Pierre Nkurikiye watu 3 ambao ni vijana wanamgambo wa chama wameuwawa maarufu Imbonerakure. "Watu wenye silaha walishambuliwa kwa kuguruneti nyumba moja katika kata ya Gikoto mtaa wa Musaga kusini mwa jiji la Bujumbura, na kuwawa watu wa 3 ambao ni vijana Imbonerakure. Wengine wa 3 walijeruhi"

Msemaji huyo wa wizara ya usalama ameongeza kuwa Polisi imeendesha msako katika eneo hilo mchana kutwa wa leo na kuwatia nguvuni watu zaidi ya 30.

Shambulio jingine lilitokea katika eneo la  kamenge kaskazini mwa jiji la bujumbura, ambapo mkuu wa idara ya ujasusi ameripotiwa kuponea chupu chupu huku. Huku mtu mmoja akiuwawa.

Amida ISSA DW BUJUMBURA
Mhariri: Yusuf Saumu