1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

NURENBERG: Ujerumani yakubali kutoa vibali vya kuishi nchini Ujerumani wakimbizi laki nne

17 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCro

Mawaziri wa mambo ya ndani kutoka majimbo 16 yanayounda muungano wa Ujerumani wanaokutana mjini Nuremberg, wamefikia maridhiano juu ya mpango wa serikali ya muungano ya kuwapatia wageni kiasi ya 200,000 vibali vya kuishi nchini Ujerumani.

Wageni hao ambao ni wakimbizi waliomba hifadhi nchini Ujerumani wakakataliwa ila hawakurudishwa nyuma. Chini ya makubaliano hayo, 20,000 ambao tayari wana kazi wataruhusiwa kuomba kibali cha kuishi nchini Ujerumani bila kupoteza muda.

Wengine 40,000 watapewa muda wa kufikia mwezi Septemba mwaka ujao wawe wamepata kazi kabla ya kuweza kuomba kibali cha kuishi nchini Ujerumani.