1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Nyuma ya mikorofoni – Vyombo vya habari na maelezo

20 Mei 2010

Je, umewahi kujiuliza yale yanayotokea wakati wa utayarishaji wa vipindi uvipendavyo vya redio au televisheni? Sasa Noa Bongo inakupa fursa ya kufahamu vyema yote yanayotokea

https://p.dw.com/p/NSrT
Radio husikika hata katika vijiji vilivyo mbali kabisa na mijiPicha: LAI F

Wao hutuletea habari kemkem kuhusu kashfa mbalimbali, kukutana na watu mashuhuri na pia huwa hawakosekani mahali popote jambo linapotokea. Uandishi wa habari ni taaluma nzuri na ya kusisimua - lakini pia inayozungukwa na vihoja vyake. Na hiyo ndio hali inayoikumba sekta ya usanii. Mfano nchini Nigeria, sekta ya filamu inazidi kuimarika kila kukicha huku maelfu ya waigizaji wakibadilika na kuwa watu mashuhuri maishani. Lakini bado watu wengi hawafahamu ugumu wa kuwa muigizaji.

Hii ni fursa nzuri ya kujifunza mengi kuhusu ulimwengu wa habari kupitia vipindi vya Noa bongo vinavyoangazia sekta hii ya vyombo vya habari. Katika vipindi hivi tutachunguza yale yanayoendelea wakati wa utayarishaji wa vipindi.
Kutana na Young Junior, Sister P, Charlie na Ezra, vijana kutoka Afrika, katika mfululizo wa vipindi kumi kwenye mchezo huu wa redio wanapojifunza mengi wanayohitaji kuyafahamu kabla ya kuanzisha kituo cha redio na kukiendeleza. Pia utasikia yote kuanzia umuhimu wa kudumisha maadili ya uandishi wa habari hadi kufikia kiwango cha kutangamana na watu mashuhuri.

Vipindi vya “Learning by Ear” ‘ Noa bongo Jenga Maisha yako’ vinasikika katika lugha sita; Kingereza, Kifaransa, Kiswahili, Kihausa, Kireno na Amharic. Na kufadhiliwa na wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani