1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ahimiza ushirikiano mpya na China

8 Juni 2013

Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito wa kuwa na utaratibu mpya wa ushirikiano kati ya Marekani na China wakati akimkaribisha rais Xi Jinping katika mazungumzo ya siku mbili katika jimbo la California.

https://p.dw.com/p/18m4u
U.S. President Barack Obama meets Chinese President Xi Jinping at The Annenberg Retreat at Sunnylands in Rancho Mirage, California June 7, 2013. Obama said on Friday he welcomed the "peaceful rise" of China and that, despite inevitable areas of tension, both countries want a cooperative relationship, as he and Xi kicked off two days of meetings. REUTERS/Kevin Lamarque (UNITED STATES - Tags: POLITICS TPX IMAGES OF THE DAY) eingestellt von qu
Mkutano kati ya rais Xi(kushoto) wa China na Obama (kulia) jimboni CaliforniaPicha: Reuters

Obama alikiri kuwa kuna masuala yanayopingana kati ya mataifa hayo mawili, ikiwa ni pamoja na udukuzi katika mtandao wa internet na masuala ya kibiashara, lakini amesisitiza kuwa kuna maeneo kadha ambayo nchi hizo mbili zinaweza kushirikiana.

"Hakuna shaka kuwa kuna maeneo yanayoleta mivutano baina ya nchi zetu mbili, lakini kile nilichojifunza katika muda wa miaka minne iliyopita ni kwamba watu wa China na Wamarekani wanataka uhusiano imara wa ushirikiano ," Obama amesema.

SAN JOSE - JUNE 29: U.S. President Barack Obama speaks about Affordable Care Act at The Fairmont Hotel on June 6, 2013 in San Jose, California. Obama was trying to spur people to sign up for health insurance in California, the nations largest health insurance market, with hopes of convincing younger people to enroll in order to keep the price down. (Photo by Stephen Lam/Getty Images)
Rais Barack ObamaPicha: Getty Images

Marais watambua

Kuna hali ya kutambua kwa upande wa marais wote Xi na mimi binafsi kuwa ni katika maslahi ya nchi zetu kufanya kazi kwa pamoja kupambana na changamoto za dunia ambazo tunakabiliwa nazo."

Xi ameyaita mazungumzo hayo "sehemu ya kihistoria ya kuanzia," akidokeza kuwa kukutana muda mfupi tu baada ya yeye kuchukua madaraka mwezi Machi kunaashiria umuhimu wa mahusiano ya nchi hizo mbili.

"Wakati nilipotembelea Marekani mwaka uliopita, nilisema kuwa bahari kubwa ya Pacific ina nafasi ya kutosha kwa mataifa haya mawili ya China na Marekani. Bado naamini hivyo," Xi amesema.

Wakati wanajaribu kuleta uhusiano mpya wa mataifa hayo makubwa yenye nguvu , vikwazo kama shutuma za Marekani kuhusu udukuzi katika mtandao wa internet kuhusiana na miundombinu ya kijeshi na wizi wa mbinu za kutengeneza bidhaa zinaweza kurejesha hali ya kutoaminiana.

US President Barack Obama speaks alongside Chinese Vice President Xi Jinping (C) during meetings in the Oval Office of the White House in Washington, DC, February 14, 2012. Obama received the 58-year-old Chinese leader-in-waiting in the Oval Office, following Xi's meetings earlier in the day at the White House with Vice President Joe Biden and Secretary of State Hillary Clinton. AFP PHOTO / Saul LOEB (Photo credit should read SAUL LOEB/AFP/Getty Images)
Mkutano kati ya China na Marekani. Rais Xi(kushoto) na Obama(kulia)Picha: SAUL LOEB/AFP/Getty Images

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili masuala kadha kuanzia matatizo ya uimarishaji wa mikakati yao ya uhasama hadi katika mahusiano ya kibiashara pamoja na mpango wa kinuklia wa Korea ya kaskazini.

"Marekani inakaribisha China inayoinukia kwa amani kama taifa lenye nguvu duniani," Obama amesema. "Kwa hakika , ni kwa maslahi ya Marekani kwamba China inaendelea katika njia ya mafanikio."

Hakuona haya hata hivyo kutaja wasi wasi wa Marekani juu ya usalama katika mtandao wa internet, na haki za binadamu nchini China pamoja na umuhimu wa biashara huru na ya haki.

Udukuzi katika mtandao

Mashambulizi katika mtandao wa internet ni suala linaloongeza wasi wasi kwa umma wa Marekani baada ya ripoti ya hivi karibuni ya serikali kudai kuwa kuna mashambulizi kutoka China dhidi ya miundo mbinu ya jeshi na biashara. Wiki iliyopita , waziri wa ulinzi Chuck Hagel ameyaita mashambulio hayo kuwa yanaleta wasi wasi katika jeshi na yanahitaji kushughulikiwa haraka iwezekanavyo.

Symbolbild zu "Muktimedia Auge Cyberwar Cyberattacke" Copyright: Fotolia/Kobes Bild: Fotolia / Kobes #23658900
Ishara ya jicho katika mtandao, ishara ya vita vya internetPicha: Fotolia/Kobes

Maafisa wa Marekani wana matumaini suala hilo halitatawala majadiliano ya marais hao, yakielekea zaidi katika masuala kama mpango wa Korea ya kaskazini wa kinuklia, mizozo ya kuwania maeneo ya ardhi katika eneo kuzunguka mataifa karibu na China na wasi wasi wa Marekani juu ya haki za binadamu nchini China. Obama pia ana matumaini kujifunza mengi juu ya mageuzi ya kiuchumi ndani ya China yanayotarajiwa kufanywa na rais Xi.

Cyberkriminalität
Ishara ya wadukuzi(Hackers) katika mtandao wa internetPicha: Fotolia

China inatarajia ziara ya Xi kulenga katika kujenga mahusiano na Obama, pamoja na masuala muhimu maalum ambayo Obama huenda atayaweka mbele ya mazungumzo hayo , kama usalama wa mtandao wa internet, Korea ya kaskazini , na mvutano wa hivi karibuni kati ya China na Japan kuhusiana na visiwa vinavyogombaniwa na mataifa hayo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / dpae

Mhariri: Daniel Gakuba