1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama akamilisha ziara ya ghafla Afghanistan

Thelma Mwadzaya29 Machi 2010

Rais Barack Obama wa Marekani anaelekea nyumbani baada kufanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan hapo jana Jumapili.

https://p.dw.com/p/MgVi
Rais Obamana mwenzake wa Afghanistan Hamid KarzaiPicha: AP

Hii ni ziara yake  ya kwanza  ya taifa hilo linalozongwa na vita tangu aingie madarakani.Akiwa mjini Kabul,Rais Obama alikutana na mwenzake wa Afghanistan Hamid Karzai na akamsisitizia umuhimu wa uongozi bora kwa kupambana na rushwa na  ufisadi pamoja na kudumisha sheria. Kamanda huyo  mkuu wa jeshi  la Marekani alikutana pia na vikosi  vya nchi yake katika kambi iliyokuwa karibu ya Bagram alikowahakikishia kuwa serikali itafanya kila iwezalo ili majukumu yao yafanikiwe.Rais Obama aliutilia mkazo umuhimu wa wajibu wa Marekani  wa kuendelea kupambana na wapiganaji wa Taleban pamoja na ugaidi ulio na mafungamano na kundi  la Al Qaeda.

Obama / Afghanistan / Bagram / USA / NO-FLASH
Rais Obama akiwahutubia wanajeshi wa Marekani katika kambi ya BagramPicha: AP