1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama akutana na wanajeshi Kabul

Ali, Ramadhan20 Julai 2008

Mtetezi wa wadhifa wa Urais wa Marekani kwa chama cha Democrat,Seneta Barack Obama amekunywa chai ya asubuhi ya leo mjini Kabul na wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan.

https://p.dw.com/p/Efcq
Obama awalahki wanajeshi Kabul.Picha: AP


Seneta Barack Obama alizungumza nao juu ya maarifa yao waliopata nchini Afghanistan-nchi ambayo imejionea hivi karibuni kuzidi kwa machafuko mwaka huu.

Obama akiwa pamoja na ujumbe wa wabunge wa Marekani wa Baraza la congress,amepanga kuonana pia na Rais Hamid Karzai baadae hii leo-kwa muujibu wizara ya nje ya afghanistan ilivyoarifu.

Ziara hii ya Bw.Obama nchi za nje tangu kuteuliwa mtetezi wa kiti cha urais,itamchukua pia Iraq,Jordan,Israel,Ujerumani,Ufaransa na mwishoe Uingereza.

Madhumuni ya ziara hii ya Bw.Obama ni kukuza kipaji chake cha maarifa ya siasa za nje na kuwajibu wakosoaji wake wanaodai hana maarifa ya kuwa amirijeshi-mkuu.