1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama awataka Mamarekani kuwa makini na kitisho cha ugaidi

12 Septemba 2015

Rais Barack Obama wa Marekani jana Ijumaa(11.09.2015)katika kumbukumbu ya shambulio la kigaidi la Septemba 11,amewataka Wamarekani kuwa makini na vitisho vya ugaidi, wakati wa kumbukumbu ya miaka 14 ya shambulio hilo.

https://p.dw.com/p/1GVQB
Washington Gedenken 9/11 Obama Weißes Haus
Obama akiongoza kumbukumbu ya shambulio la Septemba 11 katika Ikulu ya MarekaniPicha: picture-alliance/AP Photo/E. Vucci

Licha ya kuwa majeshi ya Marekani "yamepiga hatua kubwa katika kuharibu shina la al-Qaeda," lakini kundi hilo la kigaidi lililohusika katika shambulio hilo ndani ya ardhi ya Marekani, "tunatambua ukweli kwamba vitisho hivyo bado vipo," Obama amesema katika hotuba iliyotangazwa moja kwa moja kwa wanajeshi wa Marekani walioko sehemu mbali mbali duniani.

Washington Gedenken 9/11 Obama Weißes Haus
Ikulu ya Marekani wakati wa kumbukumbu ya shambulio la Septemba 11.Picha: picture-alliance/AP Photo/K. Lamarque

"Nchi za Iraq na Syria, Afghanistan, kaskazini mwa Afrika, kile tulicho na hakika nacho ni kwamba tunakabiliwa na kitisho kikubwa kinachotoka kwa makundi ya kigaidi na nadharia zao za kigaidi," Obama ameonya alipohutubia taifa kutoka Fort Meade, jimbo la Maryland.

Kengele zilipigwa

Mapema jana , majira ya asubuhi , kengele zilipigwa mara tatu katika bustani ya mashariki ya Ikulu ya Marekani ya White House katika kumbukumbu ya wakati ndege yenye nambari ya usafiri 11, ikiongozwa na rubani wa al-Qaeda, ilijigonga katika jengo la kaskazini la kituo cha kimataifa cha biashara mjini New York.

Mawingu ya buluu na sauti za ndege zikitua na kuruka katika uwanja wa ndege wa taifa karibu na mahali hapo ulikumbusha maafa ya siku hiyo.

Barack Obama Gedenkfeier 9/11 in Washington
Obama akiwa amesimama katika bendera ya Marekani ikiwa nusu mlingotiPicha: REUTERS/G. Cameron

Obama na mkewe Michelle walisimama kimya chini ya bendera ya Marekani ikiwa nusu mlingoti, wakainamisha vichwa vyao na kukaa kimya kwa muda.

Obama na mkewe waliambatana na wapishi wa Ikulu, watunza bustani na wafanyakazi wengine wa ndani katika Ikulu hiyo, pamoja na walinzi wa usalama wa taifa.

Ushahidi unapatikana kila mahali

Ushahidi wa athari za shambulio la Septemba 11 uko kila mahali--kutoka beji ya Obama yenye nembo ya bendera ya taifa ya nyota na mistari, ambayo siku hizi ni maarufu kwa kila mwanasiasa wa Marekani, hadi kuwapo kwa Lisa Monaco, mshauri wa masuala ya usalama wa ndani --wadhifa ambao haukuwapo kabla ya shambulio hilo.

USA Jahrestag der Terroranschläge vom 11. September 2001
Obama na mkewe Michelle katika kumbukumbu ya Septemba 11.Picha: Getty Images

Karibu watu 3,000 walifariki Septemba 11, 2001 katika eneo linalojulikana sasa kama Ground Zero mjini New York, katika makao makuu ya wizara ya ulinzi Pentagon na katika ndege iliyotekwa nyara ambayo ilianguka katika eneo la Pennsylvania.

"Tuna waadhimisha wale tuliowapoteza. Tunawapa heshima wote waliofanyakazi kutuweka wote kuwa salama. Tuko pamoja imara kama zamani," Obama alisema baadaye katika mtandao wa kijamii.

USA Gedenken Anschläge vom 11. September 2001
Rais Obama na mkewe Michelle wakiweka shada la mauaPicha: Getty Images

Karibu muongo mmoja na nusu, Osama bin Laden ameuwawa na majeshi ya Marekani nchini Afghanistan na Iraq yamepungua, lakini hisia za Wamarekani na mshituko umepungua kidogo tu.

Mjini New York, polisi na jamaa wa wahanga wa shambulio hilo katika kituo cha biashara cha dunia walisoma majina ya wahanga katika eneo hilo la Ground Zero, ikiwa hivi sasa ni eneo la kumbukumbu ya taifa ya Septemba 11 na makumbusho.

USA Jahrestag der Terroranschläge vom 11. September 2001
Rais Obama na waziri wa zamani wa ulinzi Chuck Hagel katika kumbukumbu ya Septemba 11, mwaka 2013.Picha: AFP/Getty Images

Katika makao makuu ya wizara ya ulinzi Pentagon, familia kadhaa waliangalia wakati waziri wa ulinzi Ashton Carter akiweka shada kubwa jeupe la mauwa.

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Yusra Buwayhid