1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ashinda tena.

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyDW

South Caroline, Marekani.

Wapiga kura wa chama cha Democratic wamepigia kura seneta Barack Obama katika kinyang’anyiro cha kuwania kuteuliwa kugombea kiti cha urais kwa chama hicho katika jimbo la South Caroline.

Hilary Clinton ameshika nafasi ya pili na John Edwards ameshika nafasi ya tatu.

Obama alihitaji ushindi huu baada ya Clinton kupata ushindi mara mbili katika majimbo ya Nevada na New Hampshire.

Akishangiliwa na umati wa watu waliompigia kuwa huku wakisema tunataka mabadiliko, Obama amesema raia wote wa Marekani bila ubaguzi wanataka mabadiliko , mabadiliko ambayo yatasahihisha sera mbaya za utawala uliopo hivi sasa.

Huu ni mpambano wa mwisho kwa chama cha Democratic kabla ya siku inayojulikana kama Jumanne kuu katika muda wa siku kumi zijazo, wakati majimbo 20 yatakapopiga kura zao katika uteuzi huo wa mwanzo.

Wagombea wa chama cha Republican wanaendelea na kampeni kwa ajili ya mpambano wao katika jimbo la Florida siku ya Jumanne.