1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama ataka mtazamo mpya katika maendeleo ya kimataifa.

Halima Nyanza23 Septemba 2010

Mkutano wa siku tatu wa Umoja wa Mataifa juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia umemalizika rasmi jana, kwa Rais Barack Obama wa marekani kutoa wito wa kuwepo kwa mtazamo mpya katika maendeleo ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/PKLM
Rais Barack Obama wa marekani akipeana mkono na Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon (kushoto) kabla ya kutoa hotuba katika mkutano wa kutathmini malengo ya milenia.Picha: ap

Katika hotuba yake aliyoitoa kuufunga mkutano huo wa Umoja wa Mataifa juu ya Malengo ya Maendeleo ya Milenia, mjini New York Marekani, Rais Barack Obama ametoa wito wa kuwepo kwa mtazamo mpya katika maendeleo ya kimataifa kwa kuzingatia uwajibikaji mkubwa zaidi kwa nchi masikini, kuhakikisha msaada unatumika vizuri.

Amesema wanaweka wazi kwamba watakuwa na ubia na nchi ambazo zitakuwa na nia ya kushika uongozi, kutokana na kile alichosema kwamba kipindi ambacho maendeleo ya nchi husika yanashurutishwa kutoka katika miji mikuu ya nchi nyingine za kigeni ni lazima kikomeshwe.

New York UN Gipfel Obama NO FLASH
Washiriki wa mkutano wa Umoja wa Mataifa wa kutathmini malengo ya maendeleo ya milenia, wakimsikiliza Rais Obama, wakati wa kufungwa kwa mkutano huo.Picha: AP

Hivyo ametaka kuachwa kwa fikra zisizo sahihi kwamba maendeleo ni sadaka ama hisani tu, isiyo hudumu maslahi yao na kuipinga kasumba kwamba baadhi ya nchi, maisha zitakuwa katika umasikini wa kudumu.

Kauli hiyo ya Rais Obama  umekuja wakati amesaini sera mpya ya Marekani inayoelekeza kwamba  kwa mara ya kwanza kuongezeka kwa maendeleo ya kimataifa  katika ajenda za juu ya masuala ya nje ya Marekani na kuelezea wazi kwamba ni suala la usalama wa taifa.

Amesema mikakati ya kiusalama ya nchi yake inatambua maendeleo kama sio tu maadili muhimu, lakini pia ni miakati muhimu na muhimu pia kiuchumi.

Rais wa Marekani pia amesisitizia msimamo wa nchi yake kubadili sera zake katika kuhakikisha wanaleta maendeleo.

Malengo ya maendeleo ya mileani yalianzishwa mwaka 2000 na kuhusisha  malengo manane muhimu, yanayotakiwa kufikiwa hadi ifikapo mwaka 2015, ambayo ni pamoja na kupunguza umasikini uliokithiri na njaa, kupambana na ugonjwa wa ukimwi, kuwawezesha wanawake, kuimarisha huduma ya afya, kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi na mtoto na kuanzisha ushirikiano wa maendeleo duniani.

Ausländische Würdenträger vor dem Kongress
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf pia katika mkutano huo alizungumzia hali barani Afrika katika kufanikisha malengo ya milenia.Picha: AP

Aidha katika mkutano huo Benki ya dunia  na mashirika mengine ya kimataifa yameonya kwamba msukosuko wa kiuchumi ulioikumba dunia yameletelesha ugumu zaidi katika kufikia malengo hayo ya milenia katika muda huo uliopangwa, na hivyo kuwahimiza viongozi duniani kuchukua juhudi zaidi.

Serikali ya Rais Obama  imeahidi kutoa zaidi ya dola bilioni 100 kufanikisha malengo hayo, lakini hata hivyo katika hotuba yake hiyo ya kufunga mkutano huo hakutangaza fedha zozote.

Katika mkutano huo wa siku tatu wa kutathmini malengo ya maendeleo ya milenia, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki moon alitangaza kutoa kiasi cha dola billioni 40 kwa ajili ya kuimarisha afya ya wanawake na watoto.

Takriban viongozi  na wakuu wa serikali kutoka katika nchi 140 walihudhuria mkutano huo wa kilele wa Umoja wa Mataifa ambao umetoa wito wa kuongezwa nguvu zaidi  malengo hayo manane ya maendeleo ya milenia.

Mwandishi: Halima Nyanza(dpa)

Mhariri: Abdulrahman