1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama amewasili Jordan.

Teichmann,Torsten22 Julai 2008

Seneta Obama awasili Jordan , katika ziara yake ya mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/EhoW
Seneta Obama.Picha: picture-alliance /dpa

Mgombea kiti cha urais nchini Marekani seneta Barack Obama wa chama cha Demokratik yupo mashariki ya kati ikiwa ni sehemu ya kampeni ya kufafanua sera zake za nje.

Seneta huyo amewasili Jordan ambapo amezungumza na waandishi habari na kwa mara nyingine alisisitiza umuhimu wa kuimarisha harakati za kupambana na magaidi nchini Afghanistan. Seneta Obama ameahidi kusimama pamoja na Israel wakati wote katika kupambana na Ugaidi. Obama aliwasili Jordan baada ya ziara ya siku mbili nchini Irak.

Seneta huyo anatarajiwa kukutana na mfalme Abdullah wa pili wa Jordan ambapo watajadili mchakato wa kuleta amani katika mashariki ya kati.