1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Obama kukutana na viongozi wa Congress

13 Januari 2015

Rais Barack Obama leo anakutana na viongozi wa baraza la Congress , lakini anakabiliana na hadhara tofauti kabisa , licha ya kuwa orodha ya wageni wake hao haijabadilika.

https://p.dw.com/p/1EJaI
Boehner Obama McConnell
Spika wa bunge John Boehmer, rais Obama(2kushoto)Picha: Getty Images/Afp/Jim Watson

Mkutano wa rais Obama na viongozi wa baraza la wawakilishji na seneti ni wa kwanza tangu pale baraza la Congress linalodhibitiwa na chama cha Republican kufanya kikao chake cha kwanza wiki iliyopita.

Kiongozi wa maseneta wa chama cha Democratic Harry Reid , mshirika wa siku nyingi wa rais Obama katika baraza la seneti, alishushwa cheo katika uchaguzi wa Novemba mwaka jana na kuwa kiongozi wa wachache katika seneti. Kiongozi wa upinzani Mitch McConnel , ambaye ni mwiba katika upande wa Obama kama kiongozi wa wachache katika baraza la seneti , sasa amechukua wadhifa wa zamani wa Reid katika baraza hilo la juu.

Boehner Obama McConnell
Mkutano kati ya rais Obama na viongozi wa baraza la CongressPicha: Getty Images/Chip Somodevilla

Mazungumzo ya fursa za ushirikiano

Watu hao watatu watajiunga na spika wa bunge John Boehmer na kiongozi wa wabunge wa chama cha Democratic Nancy Pelosi katika ofisi ya rais kujadili fursa za uwezekano wa ushirikiano kati ya chama cha Democratic na Republican mwaka huu.

Hata hivyo haifahamiki bado kwamba vyama hivyo viwili vitaweza kufumbia macho tofauti zao za wazi katika masuala kadhaa na kuangalia katika maeneo machache ya msimamo wa pamoja.

Vyama vyote viwili vilimaliza uchaguzi wa muhula wa kati mwaka jana vikizungumzia kwa matarajio juu ya kufanyakazi kwa pamoja kuhusiana na mageuzi ya kodi, kukuza biashara na maendeleo ya miundo mbinu - maeneo ambayo Obama na Warepublican wanaweza kwa kiasi fulani kukubaliana.

Barack Obama und Mitch McConnell Archiv Juli 2014
Rais Obama(shoto) na kiongozi wa wabunge wa Republican bungeni Mitch McConnel(kulia)Picha: imago/UPI Photo

Lakini mwanzoni mwa mwaka huu umetamalaki kwa kiasi kikubwa na mapambano yale ambayo yanatambuliwa kuhusiana na bomba la Keystone XL, hatua za Obama kuhusu wahamiaji pamoja na sera zake za mambo ya kigeni.

Nafasi ya maafikiano

Katika muda wa wiki mbili zilizopita, Obama mara kwa mara ametishia kuchukua hatua ya kutumia kura yake ya turufu kuzuwia miswada ambayo Warepublican wameiwasilisha kama masuala yao ya umbele.

Hata hivyo , msemaji wa Ikulu ya Marekani Josh Earnest amesema kuna " mambo chungu nzima" ambayo Obama anaweza kuyafanya mwaka huu pamoja na Warepublican.

"Haina maana tutakubaliana na kila kitu - kwa hakika hilo haliwezekani," amesema Earnest. " Lakini suala ni kwamba , tutaruhusu hali ya kutokubaliana kuhusu masuala machache na kuwa chachu cha kufikiwa makubaliano mengine yote.

Jahresrückblick USA 2011 - Nancy Pelosi und John Boehner spika wa bunge la Marekani
Nancy Pelosi kiongozi wa wabunge wa Democratic na John BoehmerPicha: picture alliance/abaca

"Rais anahakika kwamba hilo halitatokea," ameongeza.

Haijafahamika wazi iwapo Reid atahudhuria kikao hicho. Anapata nafuu kutokana na maumivu yanayohusiana na mazowezi na msemaji wake amekataa kusema iwapo atakuwapo katika mkutano huo.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape

Mhariri: Mohammed Abdul Rahman