1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ombi la Kuahirishwa kwa kesi ya Kenyatta na Ruto lakataliwa

18 Novemba 2013

Viongozi wa Jubilee nchini Kenya, wameyakosoa mataifa ya Magharibi kwa kuisaliti Kenya na kwamba yamechangia kushindwa kwa hatua ya Umoja wa Afrika ya kulitaka Baraza la Usalama, kuahirisha kesi ya Kenyatta na Ruto.

https://p.dw.com/p/1AJKb
Rais Uhuru Kenyatta na makamu William Ruto
Rais Uhuru Kenyatta na makamu William RutoPicha: picture alliance/dpa

Viongozi hao wanashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinaadamu katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu ya ICC, The Hague. Grace Kabogo amezungumza na mchambuzi wa masuala ya kisiasa nchini Kenya, Barack Muluka na kwanza alitaka kujua Jubilee wametumia misingi gani kuzilaumu nchi hizo? Kusikiliza mazungumzo bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: Saumu Yusuf