1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ongezeko la joto duniani ni tishio kwa visiwa vidogo

25 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CSqY

Viongozi katika mkutano wa Jumuiya ya Madola mjini Kampala,Uganda wamesema,mabadiliko ya hali ya hewa hasa ni kitisho kwa visiwa vidogo kama Maldives na Kiribati ambavyo pia ni wanachama wa jumuiya hiyo.Taarifa ya pamoja imesema,hasara ya kutochukua hatua ya kupambana na tatizo hilo, itakuwa kubwa kuliko gharama za kuwahi kukabiliana na tatizo la ongezeko la joto duniani.Azimio la Kampala limetoa mwito kwa nchi zilizoendelea kupunguza gesi zinazochafua mazingira.

Siku ya Jumamosi,Jumuiya ya Madola yenye wanachama 53 ilimchagua mwanadiplomasia Kamlesh Sharma wa India kama Katibu Mkuu mpya wa jumuiya hiyo,akimrithi Don Mckinnon wa New Zealnd.