1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Onyo kali kwa Eritrea juu ya kuwahifadhi magaidi

9 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRf

Marekani imetoa onyo kali dhidi ya Eritrea juu ya madai ya kuwaunga mkono magaidi.

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani amesema kuwepo kwa kiongozi wa Somalia wa mahakama za kiislam mjini Asmara ni dhihirisho tosha kwamba Eritrea inawapa hifadhi magaidi.

Aidha afisa huyo wa Marekani anayehusika na masuala ya Afrika Jendayi Frazer amesema Eritrea huenda ikajikuta kwenye orodha ya nchi zinazofadhili magaidi jambo ambalo litaisababishia kuwekewa vikwazo.

Hata hivyo Eritrea imeishutumu Marekani kwa kuupotosha makusudi ukweli wa mambo.