1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

OPEC kujadili mfumuko wa bei za mafuta duniani

5 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CXQE

Mawaziri wa Mafuta wa nchi wanachama 13 wa OPEC-shirika la nchi zinazozalisha mafuta wanakutana Abu Dhabi mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu.Mawaziri hao wanajadili matokeo ya hivi karibuni kuhusika na kuongezeka kwa bei za mafuta duniani.

Iran na Libya hata kabla ya mkutano huo zilitamka kuwa hazipo tayari kuongeza uzalishaji wa mafuta. Nchi za OPEC,bila ya Irak hutoa kama mapipa milioni 27,3 kila siku moja;hiyo ikiwa ni sawa na takriban asilimia 40 ya mafuta yanayouzwa katika masoko ya dunia.