1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Oslo. Tuzo ya utibabu ya Nobel yaenda kwa wanasayansi watatu.

8 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7HY

Tuzo ya mwaka huu ya nishani ya Nobel ya utibabu imetolewa kwa wanasayansi watatu kwa kazi yao ya utafiti juu ya seli za mbegu za uzazi. Watafiti hao wa Marekani Mario Capecchi na Oliver Smithies pamoja na Muingereza Martin Evans wamepewa tuzo hiyo kwa kuendeleza teknolojia inayojulikana kama kulenga kinasaba kutokana na panya. Jopo la majaji wa tuzo hiyo wameelezea kuwa kazi ya wanasayansi hao watatu kuwa itasaidia kupanua uwelewa wa vinasaba vingi katika mbugu za uzazi, pamoja na kuzeeka. Nishani hiyo ya utibabu ni ya kwanza kwa tuzo sita kuu zitakazotolewa mwaka huu.