1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pacquiao: naheshimu uamuzi wa NIKE

19 Februari 2016

Sakata linalomkumba bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao huenda limeathiri sio tu umaarufu wake lakini pia taaluma yake ya kisiasa

https://p.dw.com/p/1Hyjf
Manny Pacquiao
Picha: picture-alliance/dpa/E.Lin

Mfilipino huyo amesema kuwa anaheshimu uamuzi wa kampuni ya kutengeneza vifaa vya michezo – NIKE wa kusitisha mkataba wake na yeye kufuatia kauli yake yenye utata aliyosema kuwa “mashoga ni wabaya zaidi kuliko wanyama”. Nike ilisema katika taarifa kuwa matamshi wa Pacquaio yalikuwa ya “kuchukiza”.

Pacquiao ameongeza kuwa anatafuta kampuni nyingine zitakazofadhili jezi zake za masumbwi. Nyota huyo wa ndondi nchini Ufilipino na mgombea wa kiti cha Useneta ameomba radhi akisema haungi mkono ndoa za watu wa jinsia moja, lakini haipingi jamii ya mashoga na wasagaji. "hakika sisumbuliwi na utata huo. nna furaha kwa sababu nnasema ukweli. ni vibaya sana ikiwa tutauficha ukweli, nna furaha kwa sababu watu wengi walifahamishwa kilicho cha kweli".

Ndoa za watu wa jinsia moja hazikuruhusiwi Ufilipino ambako zaidi ya asilimia 80 ya idadi ya watu milioni moja nchini humo ni Wakatoliki.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP
Mhariri: Gakuba Daniel