1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PANAMA CITY.Wananchi waunga mkono mpango wa serikali katika kura ya maoni

23 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0A

Wapiga kura nchini Panama wameunga mkono kwa wingi mpango wa serikali wa kutaka kupanua mfereji wa maji wa Panama katika kura ya maoni iliyomalizika.

Asilimia 79 ya raia wa Panama wameunga mkono mpango huo huku asilimia 21 wakipinga wazo hilo.

Wapinzani wa mpango huo waliandamana mwishoni mwa wiki kudai kuwa mradi huo utazidisha deni kubwa kwa nchi hiyo.

Serikali lakini inatetea mpango wake huo wa kupanuliwa kwa mfereji wa maji kwa ajili ya meli za kisasa zipitie katika njia hiyo wakati huu ambapo uchumi wa duniani unapanuka.