1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikt wa 16 aibariki miji na dunia Urbi et Orbi

8 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCBH

Vatican City:

Waumini zaidi ya laki moja wamemiminika katika uwanja wa peter mjini Roma kusherehekea misa ya pasaka iliyoongozwa na kiongozi wa kanisa katoliki Benedikt wa 16 .Katika mahubiri yake kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni amezungumzia huzuni kutokana na shida wanazokabiliana nazo wakaazi wa ulimwengu wa tatu.Ametilia mkazo zaidi mizozo barani Afrika akikumbusha maafa katika jimbo la kusini mwa Sudan-Darfur.Kiongozi wa kanisa katoliki ulimwenguni amezungumzia pia jinsi binaadam wanavyotaabika kutokana na mizozo nchini Somalia na Zimbabwe pia.Kuhusu hali ya mashariki ya kati,Papa Benedikt wa 16 amesema “kumechomoza ishara za matumaini mema katika mazungumzo kati ya Israel na utawala wa ndanai wa Palastina.Baada ya misa ya pasaka,Papa Benedikt wa 16 amewatumia pongezi walimwengu kwa lugha 60 na kuubariki mji na dunia Urbi et Orbi.”