1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Benedikt

Mtullya, Abdu Said16 Aprili 2008

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Benedikt wa 16 ameanza ziara ya situ sita nchini Marekani.

https://p.dw.com/p/Digw
Papa mtakatifu Bedikt wa 16 ziarani nchini Marekani alipokewa na rais G.W.BushPicha: AP


Kiongozi wa  kanisa  katoliki baba mtakatifu,  Benedikt  wa 16 amesema amefedheheshwa sana  na matendo ya makasisi  wa kanisa katoliki wa nchini Marekani  ya kuwafanya vibaya watoto .


Baba mtakatifu  ameeleza hayo kabla ya kuanza  ziara  yake ya kwanza nchini Marekani kama  kiongozi wa kanisa katoliki

Amesema anaazimia kuwazuia waharibifu wa watoto kuwa makasisi. Papa Benedikt wa 16  ameeleza    kuwa waharibifu  hao  watatengwa kabisa na kanisa.

Katika  ziara yake nchini Marekani baba mtakatifu  Benedikt  wa 16  atahutubia Umoja wa Mataifa , ataendesha  sala mbili, pia atasali kwenye  sehemu iliyoshambuliwa na magaidi tarehe 11 mwezi  septemba  na  atatembelea sinagogi.

Wakati huo huo leo papa  Benedikt wa 16  anatimiza umri wa miaka 81.