1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Papa Francis awalaani magaidi

Admin.WagnerD25 Septemba 2015

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema haki ndio msingi wa maendeleo ya mwanadamu. Baba Mtakatifu amesema hayo katika hotuba aliyoitoa kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Matifa mjini New York

https://p.dw.com/p/1Gdit
Papa Francis akihutubia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
Papa Francis akihutubia kwenye Baraza Kuu la Umoja wa MataifaPicha: Getty Images/AFP/D. Reuter

Papa Francis amesema hakuna mtu,jamii, au kikundi cha watu chenye haki ya kuzihujumu haki za wengine.

Katika hotuba yake Papa Francis pia alizungumzia juu ya umuhimu wa kuyalinda mazingira. Amesema uroho wa kupita kiasi wa kutaka madaraka na mali unayadhuru mazingira na pia unawadhuru masikini.

Hapo awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alimlaki Baba Mtakatifu kwa kuisitiza kwamba kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki analihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wakati ambapo viongozi wa dunia wamekutana ili kuyapitisha malengo ya maendelea ya dunia .
Katibu Mkuu amesema wakati wote Papa Francis amezungumzia juu ya mwabatano baina ya mazingira,ustawi wa uchumi,haki za kijamii na ustawi wa binadamu.

Katika hotuba yake Baba Mtakatifu ameisitiza juu ya haja ya kudumisha amani na kulishughulikia janga la wakimbizi. Papa Francis pia ametoa mwito juu ya kuimarisha juhudi za kupambana na umasikini duniani na amesisitiza juu ya dhima ya serikali katika kuutatua mgogoro wa ukimbizi.

Papa Francis ametoa pia ametoa mwito wa kuleta haki na kukomesha matumizi ya nguvu. Amewataka viongozi wa dunia wayalinde mazingira. Pamoja na kuwapongeza kwa kuadhimisha mwaka wa 70 tangu kuundwa kwa Umoja wa Mataifa Papa Francis amewataka viongozi hao waleta mageuzi katika Umoja huo ili uweze kufanya kazi kwa ukamilifu na hivyo kuweza kuwa na ufanisi katika kuondoa madhila duniani.

Amesema yaliyotokea katika miaka 70 iliyopita yameonyesha wazi kwamba mageuzi ni jambo la lazima ili kuweza kulitekeleza lengo kuu la kuzipa nchi zote haki ya kushiriki katika mchakato wa kupitisha maamuzi.

UNO-Generalsekretär Ban Ki-moon UN New York
Picha: Reuters/M. Segar

Juu ya suala la kutoa ujauzito Baba Mtakatifu amesisitiza utukufu wa maisha ya mwanadamu.

Baba Mtakatifu pia amezumguzia juu ya sehemu za dunia ambako watu wanaandamwa kutokana na imani zao za kidini.

Masuala hayo yanaakisi hadhi yake kubwa duniani na mtazamo wake wa kuwa pamoja na watu.

Papa Francis aliekuwa kiongozi wa kwanza wa kanisa katoliki kulihutuba Bunge la Marekani amewahutubia viongozi wa dunia wanaotarjiwa kuyapitisha malengo mapya juu ya kupambana na umasikini na kuyalinda mazingira.

Kiongozi huyo wa wakatoliki amezitaka nchi tajiri ziifungue mipaka yao na kuwapokea wahamiaji wanaotafuta maisha bora.

Papa Francis alishangiliwa na wabunge wa Marekani alipoutoa ujumbe huo hapo jana.

Lakini pia aliwakumbusha wabunge wa Marekani juu ya misingi ya jamii ya Marekani inayotokana na wahamiaji.

Wabunge hao walimshangilia Baba Mtakatifu licha ya kutokubalina na baadhi ya miito yake.

Katika hotuba yake kwenye Bunge la Marekani Baba Mtakatifu pia aliyazungumzia mazingira yoliyosababisha mgogoro mkubwa wa wakimbizi usiokuwa na mithili tangu kumalizika vita kuu vya pili.

Alisema baadhi ya migogoro imesababisha kuuliwa kwa wakristo na jamii nyingine ndogo za kidini.

Ameelezea wasi wasi mkubwa juu ya mauaji hayo lakini pia ametaka busara itumike katika juhudi za kuwakabili watu wenye itikadi kali.

Baba Mtakatifu atakwenda kwenye kumbukumbu ya mashambulio ya kigaidi ya tarehe 11 mwezi septemba.