1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Ghasia zaendelea kufuatia ushindi wa Sarkozy

9 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3r

Nchini Ufaransa,ghasia zimeendelea katika miji mbali mbali,kwa usiku wa tatu kwa mfululizo baada ya kiongozi wa kihafidhina Nicolas Sarkozy kushinda uchaguzi wa rais wa siku ya Jumapili. Maandamano ya kumpinga Sarkozy yamefanywa mji mkuu Paris na katika miji ya Lyon,Nantes na Toulouse.Viongozi wa Kisoshalisti wametoa mwito wa kuwa na utlivu.Kwa hivi sasa,rais-mteule Sarkozy aliekuwa waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,anapumzika nchini Malta kabla ya kushika rasmi wadhifa wake mpya hapo tarehe 16 mwezi Mei. Msemaji wake amesema,Sarkozy atatumia muda huu wa mapumziko kupanga baraza lake la mawaziri.