1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Jaji Jean- Louis Bruguière atoa waranti wa kukamatwa baadhi ya maafisa wa serikali ya Rwanda

24 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCps

Jaji wa Ufaransa, Jean-Louis Bruguière, ametoa waranti wa kukamatwa maafisa 9 wa serikali ya Rwanda, wanashukiwa kuhusika na mauaji ya aliyekuwa rais wa Rwanda, Juvenal Habyalimana, mwaka 1994.

Maafisa hao 9 ni watu wa karibu na rais wa Rwanda Paul Kagame ambao kulingana na jaji Jean-Louis Bruguière, ndio walitoa amri ya kudunguliwa ndege ya Juvenal Habyalimana, ambayo marubani wake walikuwa ni wafaransa.

Rais wa Rwanda, Paul Kagame, ametupilia mbali madai hayo ya jaji Bruguière na kusema kuwa yamechochewa kisiasa.

Uhusiano kati ya Ufaransa na Rwanda ulikuwa na matatizo kwa miaka kadhaa, rais Kagame akiishitumu Ufaransa kuwa haikufanya lolote kuzuwia mauaji ya kuangamiza jamii yaliosibu Rwanda mwaka 1994 ambapo watutsi na wahutu wa msimamo wa wastani waliuawa.