1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS :Kampeni za uchaguzi ziko mkondo wa mwisho

15 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9i

Kampeni za uchaguzi wa rais nchini Ufaransa zinaingia wiki yake ya mwisho hii leo huku Nicolas Sarkozy wa chama cha Conservative akionekana kuwa mstari wa mbele.Mpinzani wake mkuu Bi Segolene Royal anashikilia kuwa Ufaransa iko tayari kuwa na rais wa kwanza wa kike.Kulingana na kura za maoni Bwana Sarkozy,Waziri wa mambo ya ndani wa zamani anaongoza kwa silimia kadhaa tangu mwanzoni mwa mwaka japo Bi Royal anajiamini.Bi Royal ambaye ni mwanasheria ni mama wa watoto wane na kulingana na Gazeti la Dimanche,anaamini kuwa atashinda.Kura ya maoni iliyotolewa hii leo inakanusha hilo.

Kwa mujibu wa shirika la Ipsos la gazeti la Le Point,Sarkozy huenda akapata asilimia 29 ya kura katika awamu ya kwanza ya Aprili 22 akifuatiwa na Bi Segolene Royal kwa asilimia 25 na Francois Bayrou.Francois Bayrou anahidi kuleta pamoja wafuasi wa vyama vya mrengo wa kulia na kushoto jambo linalompa nafasi ya tatu kwa asilimia 17.5 ya kura zote.Kura hiyo ya maoni ilifanywa tarehe 12 hadi 14 mwezi huu.