1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Mataifa makubwa kuzungumzia Dafur

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBoi

Mataifa makubwa kukutana mjini Paris Ufaransa hapo kesho katika jaribio la kuwa na itikio moja la kimataifa kuhusiana na umwagaji damu unaoendelea kwenye jimbo la Dafur nchini Sudan licha ya kwamba Sudan yenyewe haihudhurii mkutano huo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice tayari amewaili mjini Paris kwa mkutamo huo ambao pia utahudhuriwa na maafisa waandamizi wa serikali ya Ufaransa,Marekani,Urusi,Misri na China nchi ambazo zimekuwa zimekuwa zikisita kuwekewa vikwazo kwa serikali ya Sudan mmojawapo ya wasambazaji wake wakubwa wa mafuta.

Mkutano huo unafanyika baada ya Sudan kukubali hapo tarehe 12 mwezi wa Juni kuwekwa kwa kikosi mchanganyiko cha wanajeshi na polisi zaidi ya 20,000 wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kulinda amani huko Dafur lakini wanadiplomasia wengi wana mashaka iwapo Sudan itatekeleza ahadi yake hiyo.

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amelipa kipau mbele suala la Dafur kutokana na wasi wasi kwamba hali ya kutokuwepo kwa utulivu itaenea katika nchi jirani za Chad na Afrika ya Kati ambazo ni washirika wawili wa Ufaransa katika kanda hiyo.