1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Mpango wa ujenzi wa kinu cha kinyuklia cha nishati ya jua

22 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCqT

Nchi 30 zimesaini mkataba juu ya mpango wa kujenga kinu cha kinyuklia kikubwa kabisa duniani ambacho kitaweza kutumia nishati inayotolewa na jua.

Kufikia lengo hilo, itabidi hali ya ujoto ndani ya kinu hicho ifikie nyuzi milioni 100 kwa kipimo cha Celsius.

Umoja wa Ulaya, Marekani, Rushia, Japan, Korea ya kusini na India, zimekubali kuchangia kwa gharama na wataalamu kufanikisha mpango huo utakaogharimu bilioni 10 za Euro. Ujenzi unatarajiwa kuanza mwaka 2008 na kumalizika mwaka 2018. Wanasayansi wanasema ikiwa mpango huo utafanikiwa, kinu hicho kitaweza kuzarisha nishati safi na siokuwa na mpaka.