1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Mwanamke wa kwanza ajitangaza kugombea urais.

1 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD7E

Waziri wa zamani wa masuala ya familia na Msoshalist Segolene Royal ametangaza kuwa mgombea wa kiti cha urais nchini Ufaransa kwa ajili ya uchaguzi utakaofanyika mwakani.

Uchunguzi unamuonyesha Royal kuwa ni mgombea wa upande wa mrengo wa shoto anayeongoza ambaye atapambana na mhafidhina na waziri wa mambo ya ndani wa serikali ya sasa Nocolas Sarkozy.

Wagombe wengine kutoka katikla kambi ya Wasoshalist , kama Jack Lang na laurent Fabius , wanao muda hadi siku ya mwisho , Jumanne ijayo kuweza kutangaza iwapo watagombea.

Katika mwaka 2002 mgawanyiko upande wa mrengo wa shoto ulisaidia kumsukuma kiongozi wa mrengo wa kulia mwenye msimamo mkali Jean Marie Le Pen kuingia katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais ambapo alishindwa na rais wa sasa mhafidhina Jacques Chirac.