1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Rais Chirac hatogombea uchaguzi mwezi ujao

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCK2

Rais Jacques Chirac wa Ufaransa amethibitisha kuwa hatogombea uchaguzi wa rais utakaofanywa mwezi ujao,kubakia madarakani kwa awamu nyingine. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 74 alitoa tangazo hilo alipohotoubia taifa kwenye televisheni.Rais Chirac ataondoka madarakani mwezi wa Mei baada ya kuwepo kwenye jukwaa la kisiasa kwa zaidi ya miaka 40.Rais mpya wa Ufaransa atachaguliwa katika duru mbili za chaguzi zitakazofanywa tarehe 22 April na Mei 6.