1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy aidhinishwa kugombea urais

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaU

Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy ameidhinishwa kuwa mgombea wa wadhifa wa urais wa chama cha UMP. Sarkozy, ambaye alikuwa mgombea pekee chamani, alitumia hotuba yake katika mkutano wa chama mjini Paris kueleza mpango wake wa kampeni. Amesisitiza umuhimu wa kazi na kuahidi kurejesha mamlaka na dhima nchini Ufaransa.

Kwa mujibu wa kura ya maoni, Sarkozy ni mwanasiasa pekee wa chama cha kikosavativ anayeweza kumshinda mgombea mwanamke wa wadhifa wa urais, Segolene Royal, wa chama wa kisoshalisiti.