1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS: Sarkozy ameapishwa rais mpya wa Ufaransa

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1V

Enzi mpya imefunguliwa nchini Ufaransa baada ya mhafidhina Nicolas Sarkozy kumpokea Jacques Chirac madaraka ya urais katika sherehe iliyofanywa mji mkuu Paris.Sarkozy alie na miaka 52 alikagua gwaride la Walinzi wa Jamhuri mbele ya makao rasmi ya rais,kabla ya kupokewa na Chirac na kushindikizwa ndani ya jengo hilo kwa mkutano wa faragha.Chirac,mwenye umri wa miaka 72 ameondoka madarakani baada ya kuwa rais wa Ufaransa kwa miaka 12.Mhafidhina Sarkozy aliemshinda Segolene Royal wa chama cha Kisoshalisti katika uchaguzi wa tarehe 6 Mei ameahidi kuiongoza Ufaransa katika enzi mpya ya mageuzi.Kiongozi huyo mpya wa Ufaransa, anatazamiwa kumteua mhafidhina wa wastani, Francois Fillon kama waziri mkuu na kutangaza baraza la mawaziri wengine siku ya Ijumaa.Baada ya kuapishwa kama rais wa Ufaransa,Sarkozy ataelekea Berlin nchini Ujerumani kukutana na Kansela Angela Merkel ambako atasisitiza umuhimu wa uhusiano wa Ufaransa na Ujerumani.