1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Sarkozy ataka vikwazo vikali dhidi ya Iran

21 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNw

Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa amesema ataunga mkono vikwazo vikali zaidi dhidi ya Iran kutokana na kugoma kwake kusitisha shughuli zake za nuklea.

Akizungumza kwenye mahojiano ya televisheni ya Ufaransa Sarkozy pia ameishutumu Iran kwa njia isio ya moja kwa moja kwa kutaka kutengeneza silaha za nuklea.Hata hivyo amesisitiza kwamba Ufaransa haitaki kuona hali hiyo ya mvutano inapelekea kuzuka kwa mzozo wa kijeshi.

Wakati huo huo Rais George W. Bush wa Marekani amewaambia waandishi wa habari kwenye Ikulu ya Marekani anataraji Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litazidisha shinikizo kwa Iran katika juhudi za kufikia usuluhishi wa kidiplomasia.

Kauli hiyo ya Bush inakuja siku moja kabla ya Ujerumani na nchi wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama kukutana mjini Washington kujadili mpango wa nuklea wa Iran.