1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Sarkozy azuru Chad kuhusiana na mtoto wa watoto.

4 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/C7A0

Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amewasili nchini Chad leo ili kujadili kukamatwa kwa watu 16 kutoka mataifa ya Ulaya ambao wanashutumiwa kwa kuwateka nyara watoto.

Raia hao wa Ufaransa, Hispania na Ubelgiji wanashikiliwa kwa kuhusika na jaribio kinyume na sheria la kuwateka nyara watoto zaidi ya 100 kutoka Chad. Sita kati ya watu hao waliokamatwa ni wafanyakazi wa taasisi ya kutoa misaada ya Zoe’s Ark , ambayo inasema kuwa watoto hao hawana wazazi na wanatoka Darfur. Lakini mashirika ya kimataifa ya kutoa misaada yameonyesha shaka juu ya madai hayo. Watoto hao wanasemekana kuwa wanatoka Chad. Wakati huo huo waziri mkuu wa Ufaransa Francois Fillon ametaka ufanyike uchunguzi rasmi juu ya suala hilo.