1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PARIS : Siniora yuko Paris kwa mkutano wa wafadhili

25 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCYA

Waziri Mkuu wa Lebanon Fouad Siniora yuko Paris Ufaransa kuhudhuria mkutano wa wafadhili unaofanyika leo hii kwa lengo la kuisadia kuijenga upya Lebanon kufuatia vita vya mwezi mmoja majira ya kiangazi yaliopita kati ya Israel na wanamgambo wa Hezbollah.

Umoja wa Ulaya umeahidi kutowa euro milioni 400 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.Rais wa Ufaransa Jaques Chirac ametangaza kwamba itaongeza mkopo wake wa euro milioni 500 kwa Lebanon.Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice pia ametangaza ahadi ya kutowa dola milioni 770 za msaada mpya kwa Lebanon na kufanya msaada wa jumla wa Marekani kwa Lebanon kupindukiwa dola bilioni moja tokea mwezi wa Augusti mwaka jana.

Mgomo wa taifa ulioitishwa na kundi la Hezbollah hapo Jumatatu takriban ulisitisha shughuli zote nchini Lebanon na watu 3 waliuwawa na zaidi ya mia moja kujeruhiwa katika mapambano kati ya wafuasi wa Hezbollah na wa serikali.