1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Paris. Ufaransa huenda ikaondoa majeshi Afghanistan.

20 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0m

Ufaransa imesema itaangalia upya uwekaji wa vikosi vyake maalum vya jeshi nchini Afghanistan.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Alliot-Marie hata hivyo amekataa kuthibitisha ripoti ya gazeti moja la Ufaransa kuwa nchi hiyo inapanga kuwaondoa wanajeshi wake kutoka kusini mwa Afghanistan mwanzoni mwa mwaka ujao.

Akizungumza baada ya mkutano wake mjini Washington na mwenzake wa Marekani , Donald Rumsfeld , Alliot_Marie amesema hatua hiyo ya kuangalia upya ni hatua ya kawaida baada ya NATO kuchukua udhibiti wa nchi hiyo mwezi huu.

Kiasi wanajeshi tisa wa Ufaransa wameuwawa katika mapigano nchini Afghanistan. Tangu mwezi Julai, mashambulizi yanayofanywa na watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa Taliban dhidi ya majeshi ya kigeni nchini Afghanistan yameongezeka.

Wakati huo huo watu wanaoshukiwa kuwa ni wapiganaji wa Taliban wamewapiga risasi wafanyakazi wanane wanaofanyakazi katika kituo cha kijeshi cha Marekani mashariki ya Afghanistan.